KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Diwani Chadema Atangaza Kumtambua Rais Kikwete


DIWANI wa Kata ya Dodoma Makulu kupitia Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Ali Bilingi tofauti na msimamo wa chama chake ametangaza kumtambua Rais Jakaya
Kikwete kama Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bilingi aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipofanya mahojiano maalum na Nifahamishe.com nyumbani kwake eneo la Dodoma Makulu kufuatia kuhudhuria kwake sherehe mbili za ufunguzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho kilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete na sherehe za mahafali ya kwanza ya chuo hicho ambapo Rais Kikwete alihudhuria na kutunukiwa digrii ya heshima ya sayansi ya Udaktari wa Falsafa chuoni hapo ambapo katika sherehe zote mbili Rais Kikwete alihutubia.

Alipoulizwa kwa nini hakutoka nje wakati Rais Kikwete akihutubia
ukiwa ndiyo msimamo wa Chadema, Bilingi alisema kuwa alialikwa
kuhudhuria sherehe za chuo hicho kama Diwani wa Kata ambayo chuo
hicho kimejengwa kutoka kwa Prof. Idris Kikula Makamu Mkuu wa Chuo cha
UDOM, na hakuwa na sababu za msingi za kutoka nje wakati Rais Kikwete
akihutubia.

Alisema kuwa, anamtambua Rais Kikwete kuwa Rais wa Tanzania kwa sababu ndiye aliyetangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ni Rais kwa hiyo hana kipingamizi chochote cha kutomtambua kama ulivyo msimamo wa chama chake.

Aliongeza kusema kuwa kama akisema hamtambui Kikwete kama Rais Je
akiulizwa Rais wa Tanzani ni nani atajibu nini? Na wakati Watanzania
wote na Dunia kwa ujumla wanajua Rais wa Tanzania ni Dr Jakaya Mrisho Kikwete.

Bilingi alisema inawapasa viongozi wa Chadema wayatambue matokeo ya kura za urais kama walivyoyatambua matokeo ya kura za Ubunge na udiwani, lakini waendelee na harakati zao za kudai tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya ya Tanzania huku wakijua kuwa Kikwete ndiye Rais wa Nchi hii kwa sababu Watanzania wote wanajua kuwa mgombea Urais kwa Tiketi ya Chadema Dr Wilbroad Slaa hakushinda katika uchaguzi mkuu uliopita

No comments:

Post a Comment