KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Moto wateketeza tena soko Mbeya


Brandy Nelson, Mbeya
VILIO na simanzi vilitawala katika nyuso za baadhi ya wakazi wa Jiji la Mbeya juzi baada ya Soko Kuu la Uindini, kutetekea kwa moto uliosababisha hasara kubwa ya mali na fedha.

Lakini wakati wengine wakiwa na hudhuni, kwa vibaka iliuwa ni sherehe iliyoambatana na kupora mali madukani .

Tukio hilo lilitokea saa 2:26 usiku wa juzi na moto huo, ulitanguliwa na kukatika kwa umeme, katika eneo hilo la Uhindini.


Katika hali ya kushangaza gari la kwanza la Zimamoto, lilifika katika eneo la tukio saa 2.33 siku lakini lilishindwa kuzima moto huo ambao kwa wakati huo ulikuwa haujatekeza sehemu kubwa ya soko.

Wakizungumza na Mwananchi, mashuhuda wa tukio hilo, walisema moto huo ulianza kuwaka katikati ya soko ambako kuna vibanda vya kuuzia kuku, mama lishe, nguo na maduka.

“Huu moto ulianza kuwaka upande wa kusini katika ya soko na gari la zimamoto lilifika dakika tano baada ya moto kuanza lakinigari hilo lilishindwa kuzima moto kwa sababu maji yalikuwa hayafiki kwene moto."alisema mfanyabiashara aliyejitambulisha kuwa ni Andrew Joseph

Alisema kuwa moto huo uliendelea kuwaka kwa kasi kubwa na kuyafikia maduka ya pembeni mwa soko na kwamba hata gari la pili la zima moto lilipokwenda katika eneo hilo, lilishindwa kuzima moto.
Alisema ilipofika saa 7:00 usiku tinga tinga lilifika katika eneo hilo na kuvunja baadhi ya maduka ili kutengeneza barabara iliyosadidia gari la zimamoto kufanikiwa kuingia katika eneo la soo la kuzima moto huo.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesie, alisema chanzo cha moto huo hakijajulikana na kwamba wataalam wanaendelea na uchunguzi, ili kubaini chanzo.

Alisema mambo mengine yanayofanyiwa uchunguzi ni pamoja na idadi ya watu walioathiriwa na moto huo, vibanda na maduka.

Mwakipesile alisema tayari taratibu zimeanza za kutafuta eneo lingine kwa ajili ya kuwawezesha watu walioathirika na moto huo kuendesha shughuli zao kwa muda.

“Siyo kwamba wale ambao hawajaunguliwa wataendelea na biashara zao, hapana tunaandaa utaratibu wa kuwaondoa wote ili tulisafishwe kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa soko jipya la kisasa kama ilivyofanyika Mwanjelwa,”alisema

Aidha alisema kuwa katika tukio hilo vibaka walifanya uhalifu mkubwa wa kuvunja mduka ambayo hayakufikiwa na moto na kuiba mali

No comments:

Post a Comment