KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

CCM Temeke wachongeana kwa JK


Geofrey Nyang’oro
MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ameandikiwa barua inayowataja vigogo wa chama hicho wa ngazi ya taifa na mkoa wanaodaiwa kumpendelea mmoja wa watu walioomba nafasi ya umeya wa manispaa hiyo katika mchakato wa ndani wa chama hicho.

Barua hiyo ya Novemba 30 imeandikwa na madiwani 10 wa Temeke inawataja vigogo hao kwa majina na kiwango cha fedha walizopewa.
Kwa mujibu wa barua hiyo, kigogo mmoja wa taifa na mwingine wa mkoa, kila mmoja alipewa Sh3 milioni wakati wajumbe wasiopungua 10 kila mmoja alipewa Sh2.5 milioni ili ampitishe mgombea huyo.

Barua hiyo inadai kuwa mgombea huyo wa umeya amepewa fedha na baadhi ya wafanyabiashara mashuhuri, wakiwemo wa makampuni ya mafuta wilayani Temeke na kwamba aligawa zaidi ya Sh31 milioni ili kuwaweka sawa makada wa CCM ambao wanahudhuria vikao maalumu vya kupitisha wagombea wa nafasi wa umeya.

Barua hiyo inaeleza kuwa diwani huyo kuwa ametoa fedha hizo kwa lengo la kushawishi wajumbe wa mkutano wa kamati ya siasa ya mkoa ili jina lake lipambanishwa na wagombea dhaifu na uwezo na baadaye kuthibitishwa na kamati kuu ya CCM.


Katika barua hiyo inayodaiwa kukabidhiwa Ikulu wiki hii, mwenyekiti huyo wa CCM anatakiwa aingilie kati kwa madai kuwa mpango huo umedhamiria kumpa fisadi au mtu asiyefaa nafasi ya umeya.
“Mapendekezo yaliyotolewa yamekuwa ni ya kuweka rehani umeya wa Manispaa ya Temeke kwa fisadi ama kwa watu wasio na uwezo wa kuongoza. Tunaomba kamati kuu iliangalie jambo hili kwa umakini mkubwa,” inasemeka barua hiyo.

Barua hiyo inadai kuwa wagombea ambao majina yao yanaweza kurejeshwa ni wale wasio na uwezo kielimu na hata uzoefu, jambo litakalomrahisishia ushindi.

Katika Manispaa hiyo madiwani 18 wamejitokeza kuwania nafasi ya kuongoza baraza la manispaa hiyo na kumi kati yao wanawania umeya na wanne nafasi ya naibu meya

No comments:

Post a Comment