KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Makahaba Toka China Wagoma Kuondoka Afrika


Wanawake 11 toka China ambao walidanganywa kuwa watapewa kazi nzuri nchini Ufaransa na matokeo yake kupelekwa nchini Kongo na kuzalazimishwa kufanya ukahaba, wamegoma kuiacha bishara hiyo na kurudi kwao wakidai wanapata pesa nyingi Afrika kuliko China.
Wanawake 11 toka China ambao walilaghaiwa na kulazimishwa kufanywa ukahaba katika Jamhuri ya Kongo, wamegoma kuondoka nchini humo pamoja na jitihada za polisi na ubalozi wa China kuwaokoa toka kwenye ukahaba.

Polisi toka China walisafiri kwenda Jamhuri ya Kongo kuwaokoa wanawake hao baada ya kupewa taarifa kuwa wanawake hao wamepelekwa Afrika na kulazimishwa kufanya ukahaba tofauti na walivyoahidiwa kuwa wanapelekwa Ufaransa kufanya kazi nzuri za ofisini.

Kwa mujibu wa gazeti la South China Morning Post, wanawake hao walipelekwa nchini Jamhuri ya Kongo na kufanyishwa kazi ya ukahaba kwenye baa inayomilikiwa na raia mwenzao wa China iliyopo mjini Kinshasa.

Kwa ushirikiano wa polisi wa China na wenzao wa Jamhuri ya Kongo wanawake hao walipatikana mjini Kinshasa lakini waligoma kuondoka Afrika wakisema kuwa wanatengeneza pesa nzuri Afrika kuliko kwao nchini China.

"Wanalipwa dola 100 kwa kila mteja wanayemhudumia, wanachukua dola 50 na zinazobaki zinachukuliwa na bosi wao", alisema afisa wa polisi wa China, Yin Guohai.

Mbali ya kufanya ukahaba, wanawake hao waliweza kuingiza bidhaa za bei rahisi toka China na kuziuza kwa faida kubwa nchini humo, lilisema gazeti hilo.

Takribani Wachina 6,000 wanaishi na kufanya biashara mjini Kinshasa

No comments:

Post a Comment