KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, December 13, 2010

Maji ya chupa si salama, hupoteza akili -Mbwete

IMEDAIWa kuwa maji ya kunywa yanayouzwa mitaani si salama kwa matumzi ya binadamu na kwamba watumiaji wa maji hayo watapatwa na matatizo ya akili.
Hayo yalijulikana katika uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Maji ya Chupa uliofanywa nchini na kutolewa ripoti na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Professa Tolly Mbwete jijini Dar es Salaam.



Mbwete alisema kuwa, maji hayo si salama kwa kuwa watengenezaji wa maji hayo hawapo makini na upakiaji wa maji hayo na hayapimwi katika viwango vinavyotakiwa.

Hivyo amesema watumiaji wa maji hayo yanayouzwa mitaani wataweza kupoteza afya yao ya akili kutokana na athari zitokanazo na maji hayo.

Alisema wengi wa makampuni wa maji hayo huwa makini na kufuata viwango vinavyohitajiwa pale pindi wanapozindua maji hayo na yanapokuwa sokoni muda mrefu hukiuka taratibu za Shirika la Ubora wa Viwango nchini (TBS).

Hivyo aliiomba serikali ili kukabiliana na athari hizo ni kuundwa kwa chombo huru kitakachokuwa na jukumu la kufuatilia utengenezwaji wa maji ya chupa na kutoa taarifa kwa TBS na Ewura mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment