KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, December 13, 2010

Mwanamke akutwa amekufa hotelini


DEVOTHA Samuel (30) mkazi wa Kurasini, amekutwa amekufa katika chumba cha hoteli alichokuwa amepanga pamoja na rafiki yake wa kiume katika Hoteli ya Rombo Green View, Shekilango, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kinondoni, Bw. Charles Kenyela, ilisema kuwa, mwili wa marehemu Devota ulikutwa kwenye chumba namba 410 ‘A’ katika ghorofa ya nne ya hoteli hiyo ambapo alikuwa amepanga na rafiki yake huyo ambaye hajafahamika.

Alisema mwili wa Devota ulikutwa ukiwa unaning’inia chooni kwa kutumia khanga iliyofungwa katika nondo za dirisha za choo hicho.

Aliema chanzo kamili kuhusiana na kifo hicho bado hakijafahamika na kusema upelelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo unaendelea.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam.

KATIKA tukio jingine, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha DUCE Chang'ombe, Selemani Mwaliko (21), mkazi wa Keko Magurumbasi, alikutwa amekufa chumbani kwake huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa 6 mchana huko Keko.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, alisema mwili wa marehemu huyo ulikutwa chumbani kwake ukiwa umelala kitandani

No comments:

Post a Comment