KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, December 11, 2010

Kura ya Abyei Sudan kucheleweshwa

Ramani ya jimbo la Abyei nchini Sudan. Marekani yasema kura ya kuamua mustakabal wa jimbo hili haitafanyika mwezi ujao


Msemaji wa serikali ya Marekani, Philip Crowley, amesema kuwa kura ya maamuzi kuamua mustakabal wa eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Abyei nchini Sudan haitafanyika tarehe tisa mwezi Januari.

Bwana Crowley hata hivyo amesema kwamba serikali ya marekani itaendelea kuzitia hamasa pande zote husika kutafuta suluhu kuhusu hatma ya jimbo la Abyei.


Jimbo la Abyei
Kura hiyo ilikuwa imepangiwa kufanyika ili kuamua iwapo Abyei itaendelea kuwa sehemu ya Sudan Kaskazini ama itajiunga na Kusini.

Maafisa wa serikali ya Sudan mjini Khartoum tayari walikuwa wamelalamika kwamba hapatakuwa na muda wa kutosha kuandaa kura hiyo.

Leo jumatano ndiyo siku ya mwisho ya kuwaandikisha wapiga kura.

Kura nyingine ya maoni kuamua iwapo Sudan Kusini itajitangazia uhuru inatarajiwa kufanyika tarehe tisa mwezi Januari hapo mwakani

No comments:

Post a Comment