KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, December 30, 2010
Jengo la Machinga Complex Lageuka Sehemu ya Kulala
Jengo la Machinga Complex ambalo lilizinduliwa kwa makeke mengi kukiwa na matumaini ya kupunguza msongamano wa wafanyabiashara ndogondogo katikati ya jiji, limegeuka sehemu ya kulala kutokana na wateja kugoma kwenda kwenye soko hilo.
Nchi ya Tanzania imekuwa na malengo mablimbali ya kuendeleza jamii katika harakati za kuwakomboa wananchi wake kutoka katika janga la umaskini lakini hali imekuwa sivyo ndivyo.
Hivi karibuni Serikali kupitia halimashauri ya Manispaa ya Ilala ilibuni mbinu za kuweza kuwasidia wafanya biashara ndogondogo maarufu kama wamachinga kwa kuwajengea Jengo kubwa la Kisasa ambalo huenda kwa Afrika Mashariki hakuna jengo la wafanyabiashara ndogondogo kama hilo.
Jengo hilo lipo eneo la Karume katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam likijulikana kama Machinga Complex.
Ujenzi huo ulilenga kuwatoa wafanyabiashara ndogondogo kutoka mitaani na kuwakusanya pamoja ikiwa ni pamoja na kuondoa msongamano wa watu katika jiji la Dar es Salaam, ikiwemo maeneo ya Soko la Kariakoo Mtaa wa Kongo na kwingineko.
Ujenzi wa soko hilo wengi walidhani ni ishara kubwa ya kumkomboa mtanzania hasa wale wenye kipato cha chini.
Jengo hilo sasa lina zaidi ya miaka mitatu likiwa limekamilika lakini hakuna hata watu waliohamia humo Halmashauri ya Ilala walisema kuwa watakaohamia katika jengo hilo ni watu wa hali ya chini lakini hadi hivi sasa wengi wa waliopata nafasi ni matajiri ambao mpaka sasa hawataki kuhamia humo kutokana na kukosekana kwa watu ambao bado wamejikita katika soko la Ilala ambalo hatima yake ni tarehe 6 Januari mwaka huu.
Hakuna biashara hapa hakuna wateja hakuna watu watu tunashinda tumelala na tunalipia kodi kwa mwezi tunalipia vyoo alisema mmoja wa wafanyabiashara wa mabegi ndugu Rafael Andrea.
"Hii ina maana kuwa serikali imekuwa inabuni vitu lakini haviwasaidii wananchi", aliongeza bwana Andrea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment