KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Bomu laua wanaokaribisha mwaka mpya Nigeria

Mlipuko umetokea katika baa iliyopo karibu na kambi ya jeshi katika mji mkuu wa Nigeria na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Wanajeshi wa Nigeria wakiondoa miili ya majeruhi


Mkuu wa majeshi wa Nigeria amesema bomu hilo lilikuwa limetegwa ili kuwadhuru watu waliokuwa wakisherekea usiku wa kuamkia mwaka mpya mjini Abuja. Hata hivyo hakusema nanai anahusika na mlipuko huo.

Mlipuko huo umetokea katika soko ambalo wanajeshi na raia hukutana kula na kunywa pombe.

Msemaji wa polisi amesema watu wanne wamekufa, wakati taarifa za kijeshi zimeiambia BBC kuwa watu 11 wameuawa.

Mashetani

Msemaji huyo, Oluseyi Petrini amelaumu "watu mashetani" lakini hakutaja kundi lolote kuhusika, au sababu ambazo zinawezekana kuchochea shambulio hilo.

Pia alikataa kutaja idadi ya watu waliokufa.

Televisheni ya serikali imesema watu 30 wameuawa. Lakini msemaji wa polisi Jimon Mashood amesema watu wanne wameuawa, wanaume watatu na mwanamke mmoja.

Miili mingi

Watu walioshuhudia wameiambia BBC kuwa aliona vipande vya miili ya binadamu ikiwa imetapakaa, na kushuhudia majeruhi wakiondolewa baada ya mlipuko.

"Watu walikuwa wakikimbilia kila mahali. Kulikuwa na miili mingi, ya waliokufa na pia majeruhi. Walitumia magari ya jeshi kuwaondoa," amesema mtu mmoja aitwaye Erick akikaririwa na shirika la habari la Reuters.

No comments:

Post a Comment