KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Wachimbaji madini wakabiliwa na ukosefu nguvu za kiume



Fredy Azzah
ZAIDI ya asilimia 80 ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu, wana matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume kutokana na kutumia madini ya zebaki (Mercury), bila kutumia vifaa vya kujikinga.
Pia, asilimia 75 ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi na wataalam wa maabara za shule hizo, wameathirika au wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa mbalimbali yatokananayo na matumizi ya madini hayo, huku asilimia 60 ya madaktari hasa wa meno wakikabiliwa na hatari hiyo.

Hayo yamebainishwa kwenye ripoti ya utafiti, uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la Agenda-For Development and Responsible Development, linalojishughulisha na utunzaji na mazingira na viumbe hai.
Licha ya matatizo hayo, baadhi ya mathari mengine yatokanayo na matumzi ya madini hayo, ni magojwa ya kansa, viungo vya ndani ya mwili kama figo na maini, homoni kuathirika na kushindwa kufanya kazi ipasvyo na kumbukumbu kupotea.

Utafiti huo umefanywa kanda zote za Tanzania bara, ulihusisha wachimbaji na wanunuzi wadogo wa madini ya dhahabu, shule 56 za sayansi, hospitali na vituo vya afya 43.
“Wachimbaji wadogo wa dhahabu ndio waathirika wakubwa wa madini haya, mbali na magojwa ya ngozi, madhari katika viungo vya ndani kama figo… wengi wana tatizo la nguvu za kiume ndio maana hata kule wengi wanatumia dawa za kuongeza nguvu,” alisema Haji Rehani, msimamizi wa utafiti huo.

Alibainisha kuwa, kwa kiasi kikubwa wahusika huathiriwa na madini hayo wakati wa kusafisha madini au kuyachoma.
Kwa upande wa madaktari ripoti hiyo inaonyesha, mbali na kuwa kwenye hatari ya kupata madhara hayo kutokana na kutumia vifaa kama kipima joto (thermometer) na vile vya kupima shinikizo la damu, ambavyo vina madini hayo, wale wa meno ndio wako katika hatari kubwa ya kupata madhara.

“Katika shule nyingi tulizo tembelea wale watumishi wa maabara waliofanya kazi kwa muda mrefu tulikuta wameathirika sana, wengine miili yao inatetemeka lakini wengi uwezo wao wa kumbukumbu umeshuka sana,” alisema

No comments:

Post a Comment