KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Waziri wa Mambo ya nje wa Iran amefutwa kazi

Katika tukio la kushangaza Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejeda amemuachisha kazi Waziri wake wa Mambo ya nje Manoucher Mottaki, ambaye yuko ziarani nchini Senegal. Afisa wa ngazi za juu wa masuala ya nyuklia Ali Akbar Salehi, mshirika mkuu wa Ahmedinejad ameteuliwa kushikilia kwa muda wadhifa huo

.Kulingana na tovuti moja ya wanamageuzi, imedaiwa Mottaki amekuwa akikosoa msimamo wa Ahmedinejad na ametofautiana na sera zake za nje. Wakati huo huo, Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema kuondolewa kwa Mottaki hakufai kutatiza mazungumzo kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran yanayoendelea mjini Geneva, Uswisi

No comments:

Post a Comment