KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 30, 2010

Basi latekwa, 7 wajeruhiwa


WATU saba wamejeruhiwa vibaya na kuporwa mali zao baada ya basi walilokuwa wakisafiria la Sabena kutekwa na na majambazi.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Liberatus Barlow, alisema tukio hilo limetokea juzi, majira ya saa 7 usiku kati ya eneo la Mambali na Igombe .

Alisema basi hilo lilkuwa likitokea Dar es Salam kuelekea mkoani Tabora na ilipofika wilaya Nzega eneo hilo majambazi walizuaia basi hilo kwa mawe na kufanya uharifu huo.

Kabla ya kuanza uharifu majambazi hao walimjeruhi dereva wa basi hilo aliyetambulika kwa jina la Salum Ally na kumpiga risasi sehemu zake za makalio.

Pia waliweza kuwajeruhi watu saba wakiwemo Jakson Peter, Fatma Athuman (28), Johari Yona (28), Masaga Mayunga (24), Shaban Mrisho (29) na Shukuru Kidika

Kamanda Barlow alisema simu zipatazo 20 ziliporwa zikiwemo na mali nyingine za abiria hao.
Msako unaendelea kwuabaini waharifu hao na majeruhi wamelazwa hospitali ya Iiteto

No comments:

Post a Comment