KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 30, 2010

Mtoto aliyeibwa aokotwa uchochoroni akiwa ndani ya boksi


MTOTO Twaha Masoud, mwenye umri wa miezi mitano, ambaye alipotea kwa njia ya kuibwa ameokotwa akiwa ndani ya boksi lililotupwa uchochoroni karibu na nyumba aliyokuwa akiishi na wazazi wake akiwa hai huko Mtoni.
Taarifa hii ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, ofisni kwake na kusema, mtoto huyo aliwekwa kwenye boksi na kutupwa uchochoroni na mtu ambaye hajafahamika hadi taarifa hii inatolewa.

Kamanda Missime alisema, mtoto huyo alitambuklwia baada ya kuonekana linacheza na wapiti njia wa eneo hilo na kulifungua ndipo walipomkuta mtoto huyo na baadae bi. Fatuma Hamis alipotakiwa amuangalie mtoto huyo alimtambua kuwa ndiye mwanae aliyeibiwa siku mbili nyuma.

Hata hivyo Missime alisema mama huyo alikabidhiwa mtoto huyo na juhudi za kumsaka mtuhumiwa bado zinaendelea

No comments:

Post a Comment