KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Barabara ya Mandela yaleta tafrani


KUFUATIA kero ya muda mrefu inayotokana na ujenzi wa barabara ya Mandela, wananchi wamechoshwa na hali hiyo na kupelekea kufunga barabara hiyo kwa magogo na mawe ili iweze kumalizwa na kuondoa usumbufu kwa watumiaji wake.
Jana baadhi ya watu na wale wakazi wa Tabata Matumbi waliamua kufunga barabara hiyo kwa masaa matatu ili wawezwe kusikilizwa kero zao kuhusiana na barabara hiyo.

Wananchi hao waliziba barabara hiyo kushinikiza umalizwaji wa barabara hiyo ambao umedumu kwa muda mrefu ikiwemo na kutaka kuzibuliwa kwa mtaro wa majitaka ulioziba eneo hilo na kusababisha mafuriko majumbani pindi mvua zinaponyesha.

Kufuatia hali hiyo wananci hao walitumia mawe yatumikayo kwenye ujenzi ka ajili ya kuzibia magari na baadae wanajeshi waliingilia kati na kuondoa mawe hayo na hali ilirudi kama awali baada ya wanajeshi hao kuondoka mahali hapo.

Hata hivyo polisi walifika mahali hapo na walifanikiwa kuwaondoa watu hao ambapo watu hao walisababisha usumbufu wa usairi kati ya Ubungo hadi Buguruni kwa zaidi ya masaa matatu

Ukarabati wa barabara hiyo ya Mandela umechukua muda mrefu ukarabati unaofanywa na kampuni ya Maltauro- Spencon- Stirlinga Joint Venture

No comments:

Post a Comment