KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, November 19, 2010

Wengi wafurahia uchaguzi wa PindaWANANCHI wengin walioweza kuhojiwa na mtandao huu, wameonekana kufurhia uchaguzi wa Rais Jakaya Kikwete kumrudisha madarakani Mizengo Pinda kwa kuwa alikuwa makini, muadilifu katika madaraka yake hayo.
Wananchi hao ni wake wa mkoa wa Morogoro, Dodoma, Pwani na Dar es Salaam ndio waliweza kuhojiwa na kutoa hisia zao hizo.

Wengi wao walisema, walikuwa wanategemea hilo na kusema Rais Kikwete aliona utendaji wake na ndio manda alimrudisha madarakani.

"Pinda ni mtendaji mzuri sana, tumefurahia uteuzi wake"

Nae Waziri Pinda akiongea baada ya kupitishwa bungeni humo, alisema japo na kupata kura za hapana zaidi ya 45 atashirikiana na wabunge woe hata wale waliyomkataa kwa kuwa yeye kazi yake ni kuongoza na hataangalia mapungufu yaliyopo bungeni humo.

“Ndugu zangu naahidi kushirikana na wapinzani, japo leo marafiki zangu kutoka Chadema wameninunia na jana tulikuwa wote, mimi siachukuia mtu kwani hii ni siasa, nitashirikiana na wabunge wote wala sitabagua” alisema Pinda

Pinda ambaaye anajiita mtoto wa mkulima na danajivunia hilo, anaanza majukumu yake hayo ya uongozi na kusubiria timu yake iingine iundwe na Rais Jakaya Kikwete

No comments:

Post a Comment