KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Mnyika, Lissu wamtingisha Makinda


WABUNGE wapya machachari kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu (Singida Mashariki) na John Mnyika (Ubungo), wameonekana kumtoa jasho spika kwa kumbana na kanuni anazotumia spika huyo.
WAbunbge hao ambao wameanza kwa moto wa hali ya juu bungeni humo walionekana wako makini na kanuni zitumikazo bungeni humo na kumfanya spika Anna awe katiika wakati mgumu.

WAbunge hao walianza kutoa makucha yao katika mchakato mzima wa kumthibitihsa Waziri mkuu uliowataka wapige kura ya ndio amda hapana.

Mnyika mbunge mteule wa Ubungo alimtaka spika huyo atoe ufafanuzi juu ya usiri wa karatasi za kupigia kura wka kuwa karatasi hizo zilikuwa na namba na kudai hakutakuwa na siri kwa kuwa ingefahamika nani alitoa kura ya ndio ama hapana.
Mnyika alisema uwepo wa namba aktika karatasi hizo kunaweza kumfanya mtu kujua nani alipewa karatasi namba ngapi na kura aliyopiga ili kuwa ya ndio ama hapana katika kumthibitish a waziri huyo.

Kwa upande wa Lissu alimtaka spika huyo, kutumia kanuni 53 (6)a, (6)c ambapo alisema endapo hoja itatolewa na serikali bila kupitia katika Kamati ya Kudumu ya Bunge, kiongozi wa upinzani bungeni atapata fursa ya kujadili hoja lakini Bunge halikufanya hivyo baada ya hoja ya kumuidhinisha Waziri Mkuu kutolewa

No comments:

Post a Comment