KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Nahodha aula, ateuliwa kuwa mbunge


RAIS Jakaya Kikwete amemteua aliyekuwa Waziri Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Shamsi Vuai Nahodha kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nahodha ambaye alikuwa Waziri Kiongozi katika serikali ya Rais Amani Abeid Karume.

Mbali na huyo pia Rais Kikwete aliwateua Bi. Zakia Meghji aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, na aliwahi kuwa Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya Tatu na Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, ambaye aliwania ubunge katika jimbo la Mkanyageni.

Rais Kikwete amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua wabunge 10.

Hivyo Rais Kikwete bado ana nafasi saba za kuteua wabunge ambapo ameahidi kuendelea kuteua wabunge hao katika siku zijazo.

Taarifa iliyoifikia nifahamishe ilisema kuwa, Rais Kikwete leo anatarajia kulihutubia Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano

No comments:

Post a Comment