KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Vita ya umeya Ilala moto


Geofrey Nyang’oro
KINYANG'ANYIRO cha kiti cha umeya wa Ilala jana kilizidi kupamba moto baada ya Jerry Slaa kuchukua fomu kupmabana na mkuu wake, Abuu Juma na hivyo kufanya idadi ya wanachama wa CCM wanaowania nafasi hiyo hadi sasa kuwa wanne.
Kiti cha umeya wa Ilala kinaonekana kuwa ndio kitakuwa kikubwa miongoni mwa manispaa za jiji la Dar es salaam kutokana na mpango ulioripotiwa na vyombo vya habari vya kulivunja Jiji la Dar es salaam na hadhi hiyo kuhamishiwa Ilala ambayo iko katikati ya wilaya tatu za jiji.

Meya Juma amekuwa meya wa Ilala kwa kipindi cha miaka mitano, akisaidiwa na Slaa, ambaye alikuwa naibu, lakini sasa wawili hao watapambana kuwania kiti hicho.
Slaa alijitosa jana kuwania nafasi hiyo muhimu na kuweka bayana changamoto nyingi zinazoikabili Ilala, ikiwa ni pamoja na tatizo sugu la uchafu na ongezeko la wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) kwenye mitaa ya Ilala.
“Manispaa ya Ilala ndio kitovu cha jiji; inapofikia mahali uchafu unashindwa kutoka hadi eneo zima linakosa hata sehemu ya kupigia picha, ujue uongozi wa mahali hapo una tatizo. Mimi nimeliona hilo na naamini nina uwezo wa kushughulikia hayo,” alisema Slaa ambaye leo anatarajia kurudisha fomu.

Alisema anaamini kuwa anaweza kazi hiyo kutokana na uzoefu alioupata kwenye baraza lililopita la madiwani wakati alipokuwa naibu meya wa manispaa hiyo.

Alisema katika kipindi hicho cha miaka mitano alifanikuwa kuwa mjumbe katika kamati zote za kudumu za baraza la Madiwani na pia kuongoza vikao mbalimbali vya halimashauri.
Aidha alisema aliiwakilisha manispaa hiyo katika vikao mbalimbali vya ndani na hivyo kupata uzoefu mkubwa na uwezo wa kufanya kazi hiyo.
Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Ernest Charle aliwataja madiwani wengine waliojitokeza kuwa ni Dk Didas Masaburi kutoka Kata ya Kivukoni, Salum Kisalala (Gerezani) na mbunge wa zamani wa Dodoma Mjini, Hashim Sagafu (Mchafukoge).
Charle aliwataja madiwani wawili waliochukua fomu kuwania unaibu meya kuwa ni Kheri Kessy (Kisutu) na Abdukarimu Masamaki (Kariakoo).

Kazi ya kuchaukua fomu za kwania nafasi hiyo ndani ya Chama cha Mapinduzi imeanza juzi Novemba 20 inatarajia kukamilika kesho saa 10:00 jioni.
Kwenye Manispaa ya Kinondoni pekee, hadi kufikia jana jioni madiwani 17 walikuwa wamechukua fomu, kati yao 12 wanawania kiti cha Meya wa Kinondoni, nafasi iliyoachwa wazi na Shaban Londa, wakati sita wakichukua fomu ya kuwania unaibu Meya.
Mchakato wa kumsaka meya utakamilisha safu za uongozi katika manispaa hizo baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao ulishuhudia kwa mara ya kwanza upinzani ukitwaa majimbo mawili na kuchukua nafasi mbalimbali za udiwani.

Kwenye Manispaa ya Kinondoni ambako baraza lake la madiwani litakabiliwa na upinzani mkali kutoka Chadema yenye madiwani wengi, hadi jana wanachama tisa kutoka CCM walikuwa wamejitokeza kuchukua fomu , huku watu watatu wakitokea Chadema.
Hali kadhalika nafasi ya naibu meya wa manispaa hiyo inaonyesha kuwa kuna hekaheka kubwa kuliko wakati mwingine wowote baada ya wanachama wanne wa CCM kujijitokeza kuchukua fumo huku wawili wakitokea Chadema.
Katibu msaidizi wa CCM Kinondoni, Abihudi Shilla aliiambia Mwananchi kuwa kazi ya kuchukua fomu ilianza juzi na kesho ndio mwisho na kusisitiza kuwa nafasi bado ipo kwa wanachama wanaotaka nafasi hiyo.
“Tangu tumenza kutoa fomu za umeya juzi Novemba 20 wanachama wa CCM 12 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo, tisa kati yao wanawania nafasi ya umeya na wanne wamejitokeza kwenye nafasi ya naibu huku mmoja akitokeza katika nafasi zote mbili,” alisema Shila.

Shila alitaja majina ya madiwani waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa ni Issa Mtemvu (kata ya Kibamba), Boniface Mnyachimwe (Mbweni), Othuman Bujugo ( Magomeni), Clement Bosco (Mabwepande), Majisafi Shariff (Bunju), John Mome (Wazo ), Christine Kirigiti (Msasani) na Lucas Mgonja (Ndugumbi).
Alisema katika mchakato huo madiwani wanne walijitokeza kuwania nafasi ya unaibu ambao ni Rogate Mbowe (kata ya Msasani), Hajat Husna Hemed (Kinondoni), Lucas Mgonja (Ndugumbi) ambaye pia anawania umeya na Hilda Kitana (Kwembe).
Katibu msaidizi wa CCM wilayani humo alitaja madiwani wawili ambao walichukua fomu na kuzirudisha kuwa ni John Morro kwa nafasi ya meya na Rogate Mbowe kwa nafasi ya unaibu.

Naye katibu wa Chadema wa Kinondoni, Henry Kilewo alitaja majina matatu ya wanachama waliojitosa kuwania nafasi hiyo kuwa ni Janeth Rithe, Athumani Uloleulole na Wiliamu Mwangwa.
Alisema waliochukua fomu za unaibu ni Renatus Pamba na Paschali Manota.
Kilewo aliliambia Mwananchi kuwa kazi ya kuchukua na kurudisha fomu katika chama hicho imekamilika na sasa kilichobaki ni kwa chama kupitia majina ya wagombea na kupitisha jina la atakayekwenda kupambana na wapinzani wake kutoka kutoka vyama vingine

No comments:

Post a Comment