KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Kivuko Kigamboni chasababisha maafa


Hemed Athuman na Hamad Amour (TSJ)
WATU watatu wamepoteza maisha katika matukio tofauti jijini Dar es salaam, mmoja akikandamizwa na mlango wa kivuko akiwa ndani ya gari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema kijana aliyetambuliwa kwa jina moja la Vincent, amefariki dunia kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Hiace maeneo ya Yombo Makangarawe jana saa 12:30 asubuhi.
Misime alisema polisi inaendelea na msako wa gari hilo ambalo linafanya safari zake kati ya Tandika na Yombo Buza.
Shuhuda wa ajali hiyo, Ally Ngwike, mkazi wa Yombo Makangarawe, alisema marehemu alikuwa na tatizo la akili na gari lililomgonga lilikuwa mwendokasi.

Katika tukio jingine, Misime alisema lilitokea maeneo ya feri baada ya gari aina ya Toyota pickup kugandamizwa na mlango wa kivuko cha Mv Magogoni na kusababisha kifo cha dereva wa gari hilo, Mohamed Nandumbe (58).
Dereva huyo alikuwa mkazi wa Magomeni na maiti imehifadhiwa Hospitali ya Vijibweni iliyopo Kigamboni. Mganga wa zamu wa hospitali hiyo, Dk Pili Mwera, alithibitisha kupokea mwili huo.

Wakati huohuo, Hassan Juma (25), mkazi wa Mbagala Rangi Tatu, dereva wa pikipiki aina ya Chuma alikutwa amekufa maeneo ya Mbagala Nzasa.

Mtu wa karibu na Juma, Ibrahim Kagina, alisema mara ya mwisho waliachana saa 8:00 usiku

No comments:

Post a Comment