KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Jengo la Ghorofa 30 Linapowaka Moto


Watu wanane wamefariki na watu zaidi ya 90 wamejeruhiwa baada ya mojawapo ya majengo marefu ya mjini Shanghai nchini China kuwaka moto na kupelekea baadhi ya watu wajirushe toka ghorofani kunusuru maisha yao.
Jengo la ghorofa 30 lililopo Jing'an katikati mwa jiji la Shangai, limewaka moto na kupelekea vifo vya watu wanane na watu zaidi ya 90 kujeruhiwa.

Jengo hilo ambalo lilijengwa kwenye miaka ya tisini, ni makazi ya familia zaidi ya 100.

Jengo hilo liliwaka moto kwenye majira ya mchana na kupelekea mtafaruku mkubwa ambapo baadhi ya watu waliamua kuyanusuru maisha yao kwa kujirusha toka ghorofani.

Chanzo cha moto huo kinasemekana ni moto uliozuka kwenye vifaa vya ujenzi wakati wa kulifanyia ukarabati jengo hilo.

Zimamoto walifanikiwa kuudhibiti moto huo baada ya muda mrefu kupita lakini hadi wakati huo sehemu ya juu ya jengo hilo ilikuwa imeishateketea kwa moto

No comments:

Post a Comment