KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Viongozi wa IGAD wajadili hatma ya Sudan



Wadadisi wa siasa za Sudan wanahofu kuhusu usalama wa Sudan baada kura ya



Mkutano muhimu wa viongozi wa shirika la maendeleo katika upembe wa Afrika IGAD, unafanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia kujadili usalama wa Sudan.

Mkutano huo unaoongozwa na Rais wa Kenya Mwai Kibaki, utaangazia zaidi kura ya maamuzi kuhusu uhuru wa Sudan Kusini itakayofanyika Januari, mwakani.

Rais Omar al Bashir na makamu wake Salva Kiir ambaye pia ni kiongozi wa Sudan Kusini, watawasilisha ripoti kuhusu tathmini yao ya maandalizi ya kura hiyo.

Viongozi wa Afrika mashariki, wamelenga kupata uhakikisho kuwa kura hiyo ya maamuzi itafanyika katika mazingira ya amani na matokeo yatakubalika.

Mkutano huo pia utajadili mchakato wa amani nchini Somalia

No comments:

Post a Comment