KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Janga la maafa la kumba Cambodia



Zaidi ya watu mia nne walipata majeraha mabaya katika mkasa huo


Waziri mkuu wa Cambodia, Hun Sen ametangaza kuwa alhamisi wiki hii itakuwa siku rasmi ya kitaifa kuomboleza vifo vya takriban watu mia tatu hamsini, vilivyotokea kufuatia mkanyagano uliotokea wakati wa sherehe za mwaka mpya mji mkuu, Phnom Penh.

Tangazo hilo limetolewa wakati harakati za kutambua miili ya watu walioathirika katika mkasa huo zikiendelea. Mamia ya watu pia walijeruhiwa wakati umati wa watu uliofurika kwenye kivukio kimoja ulianza kusukumana.

Bwana Hun Sen ameahidi kuwa uchunguzi utafanyika kuhusiana na tukio hilo- ambalo amelitataja kuwa mkasa mbaya zaidi kuwahi kutokea Cambodia tangu enzi ya Khmer Rouge katika miaka ya sabini.

Ameongeza kuwa serikali itawalipa jamaa za waliokufa dola 1,250 kugharamia shughuli za mazishi

No comments:

Post a Comment