KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Korea Kusini yajibu mashambulizi ya Kaskazini

Moshi ukifuka katika kisiwa cha Yeonpyeong

Korea Kusini imejibu mashambulizi baada ya Korea kaskazini kurusha mabomu kadhaa katika kisiwa kilichopo mpakani na kusababisha vifo vya wanajeshi wawili.




Jeshi la Kusini lilikuwa katika hali ya tahadhari, ya juu kabisa tangu wakati wa vita, baada ya mabomu kurushwa katika kisiwa chake cha Yeonpyeong.

Korea kaskazini imesema haikuwa ya kwaza kufanya shambulio. Wanajeshi wawili wanamaji na raia wanne pia walijeruhiwa.

Mifarakano

Wachambuzi wa mambo wanasema hii ni moja ya mzozo mkali zaidi tangu kumalizika kwa vita vya Korea, ambavyo viliisha bila ya mazungumzo ya amani mwaka 1953
Nyumba zimeteketea kisiwani humo

Kumekuwa na mifarakano ya mpakani ya hapa na pale tangu wakati huo, lakini tukio hili la sasa limekuja wakati mvutano ukizidi kukua katika eneo hio.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Il, anadhaniwa kuwa ni mgonjwa, na huku pia akijaribu kuhakikisha mwanaye anaingia madarakani.

Siku ya Jumamosi, Korea kaskazini pia ilionesha kile ambacho kinatajwa kuwa kituo cha kuchuja madini ya urani, ambacho ni kama njia ya pili ya kutengeneza silaha ya kinyuklia.

Hatua hiyo ilimfanya mwakilishi maalum wa Marekani wa masuala ya Korea kaskazini, Stephen Bosworth, kufutilia mbali kujerejelewa kwa mazungumzo ya pande sita kuhusu kuondoa silaha za nyuklia, ambazo Pyongyang iliacha kufuatilia miaka miwili iliyopita.

Mambomu 80

Msemaji wa wakuu wa majeshi wa Korea Kusini amesema mabomu ya Korea kaskazini yalianza kudondoka katika bahari nje kidogo ya kisiwa cha Yeonpyeong saa nane na nusu mchana, saa za huko.

Mabomu yasiyopungua 50 yalitua kisiwani humo, mengi yakigonga kituo cha kijeshi cha Korea Kusini. Wanajeshi wa Kusini mara moja walijibu mashambulizi, kwa kurusha mabomu 80, kama kujilinda, amesema Kanali Lee Bung-Woo.

Mkazi mmoja wa kisiwa hicho ameliambia shirika la habari la AFP kuwa nyumba kadhaa zimeharibiwa, huku picha za televisheni moshi ukifuka katika kisiwa hicho

No comments:

Post a Comment