KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

VIDEO - Paka na Mamba Nani Zaidi? Paka

Kwa kuambiwa huwezi kuamini na hata kwa walioshuhudia kwa macho yao hawakuweza kuyaamini macho yao, paka ameweza vipi kusimama kidete mbele ya mamba mkubwa kama huyu na kufanikiwa kumfanya mamba akimbilie majini.
VIDEO ya tukio hilo lililotokea mjini New Orleans nchini Marekani imekuwa gumzo la siku kwenye televisheni za Marekani.

Paka mwenye umbile la kawaida alisimama kidete mbele ya mamba ambaye binadamu mwenye akili zake asingeweza kumsogelea karibu.

Katika tukio hilo ambalo ni nadra sana kulishuhudia duniani, paka alishinda gemu kwa kufanikiwa kumtisha mamba kwa mikwara yake na kumfanya mamba akimbilie majini.

Hata baada ya mamba huyo kurudi tena na mwenzake, paka huyo aliendeleza mikwara yake na kuwatiririsha mamba wote wawili majini


No comments:

Post a Comment