KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Mgonjwa wa Akili Ambaka na Kumuua Mama Yake


Mwanaume mmoja wa nchini Kongo ambaye alikuwa na matatizo ya mtindio wa ubongo, amembaka mama yake na kisha kumuua.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa katika mji wa Kasai, Jamhuri ya Kongo, mwanaume huyo ambaye ni mgonjwa wa akili, alimuua mama yake baada ya kumaliza kumbaka.

Mgonjwa huyo wa akili alikuwa akiishi pamoja na mama yake na imeripotiwa kuwa aliutelekeza mwili wa mama yake baada ya kutimiza haja zake.

Majirani waliougundua mwili wa mama yake, waliripoti polisi na mgonjwa huyo wa akili alitiwa mbaroni lakini baadae aliachiwa huru.

Taarifa zaidi zilisema kwamba mgonjwa huyo wa akili alikuwa na tabia ya kuwabaka wanawake anapokutana nao kwenye vichaka na watu walishalalamika kwanini kichaa huyo alikuwa hawekwi kwenye hospitali za vichaa.

Baada ya kifo cha mama huyo, kumekuwa na shinikizo kubwa kwa mamlaka husika ambapo watu wamekuwa wakishinikiza wagonjwa wa akili wasiachwe wakazurura mitaani na matokeo yake kusababisha matatizo mbalimbali kwenye jamii

No comments:

Post a Comment