KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, November 11, 2010

Ugumu wa maisha wampeleka kuzimu


KIJANA Muholana Nsimanya [30 -35] mkazi wa Mwananyamala, amejiua kwa kunywa sumu kutokana na kukabiliwa na ugumu wa maisha na kuacha ujumbe kuwa anaomba azikwe kwa kufuata kanuni za dini ya kiislamu.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw. Elias Kalinga alisema kuwa, Nsimanya wakati akipita maeneo Kinondoni Makaburini alianguka ghafla na wasamaria kumkimbiza Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.

Kalinda alisema, marehemu alipofikishwa hospitalini hapo alikutwa na ujumbe uliosema” nimejiua kwa hiyari yangu mimi mwenyewe, naw wala sikuudhiwa na mtu, nimefanya hivyo kutokanda na ugumu wa maisha unaonikabili” na ujumbe huo ulimaliza naomba mnizike kwa taratibu ya dini ya kiislamu.

Kamanda Kalinga alisema pia marehemu huyo alikutwa na soda ya kopo aina ya sayona wanayoidhania kuwa ametumia kunywea smu yake hiyo.

Kalinga aliwataka kama kuna yoyote aliyepotelewa nan ndugu dama jamaa huyo ajitokeze, na kudai uchunguzi unaendelea na mwili huo umehifadhiwa hospitalini hapo na kuzikwa uchunguzi utakapokamilika

No comments:

Post a Comment