KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Wachina Wajenga Hoteli ya Ghorofa 15 Kwa Siku 6


China imethibitisha kuwa iko juu katika masuala ya ujenzi kwa kufanikiwa kujenga hoteli ya ghorofa 15 kwa kutumia siku 6 tu.
Hoteli ya ghorofa 15 imejengwa nchini China katika kipindi cha muda wa siku sita tu na tayari imeishaanza kutumika kama hoteli.

Mbali ya kukamilika katika kipindi cha muda mfupi, hoteli hiyo iliyojengwa katika mji wa Changsha, jengo lake lipo imara kiasi cha kuhimili tetemeko kubwa kabisa la ardhi iwapo litatokea.

Jengo hilo pia limetumia teknolojia za kisasa kama vile kuta zisizopitisha sauti.

Ujenzi wa jengo hilo ulifanyika kwa masaa 24 kila siku bila kupumzika kwa muda wote wa siku 6.

Ujenzi ulikamilika bila hata mfanyakazi mmoja kupata ajali kazini

No comments:

Post a Comment