KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, November 10, 2010

Spika kutangazwa keshoKESHO Bunge linatarajia kumtangaza jina la atakayekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.


Spika atakayechaguliwa atakuwa na mamlaka la kuongoza Bunge tukufu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Baadhi wa watanzania walikuwa wakiomba kwa apatikana spika atakayeweza kuliongoza bunge hilo, mwenye uwezo thabiti na atakayeweza kutetea haki za wanyonge.

Leo Kamati Kuu (CCM) kinatarajia kuketi mjini Dodoma kuchuja majina ya wagombea watatu watakaoingia katika kinyang’anyiro hicho.
Jumla ya Wanachama 13 wa CCM walijitokeza kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge.

Spika atakayepatikana ataweza kuliongoza bunge hilo la 10 kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mungu ibariki Tanzania ipate kiongozi bora katika nyanja hiyo muhimu la kulijenga Taifa hili

No comments:

Post a Comment