KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, November 10, 2010

Bi Harusi Anapovuta Bangi...maishani!


Mwanamke mmoja wa nchini Marekani amejikuta akikabiliwa na kifungo cha miaka 23 jela baada ya bangi alizozivuta kumtuma avae shela la harusi na kisha kuvamia nyumba ya jirani yake.
Baada ya kuvuta bangi, Melissa Wagaman mwenye umri wa miaka 33, bangi zake zilimfanya ajione kuwa yeye ni Bi Harusi ambaye ametoka kufunga ndoa na pia zilimfanya afikirie kuwa jirani yake amemteka mama yake na kumfungia ndani ya nyumba yake.

Melissa huku akiwa amevaa shela la harusi alivunja kioo cha dirisha la jirani yake kwa kichwa na kuingia ndani akiamini anaenda kumuokoa mama yake.

Katika tukio hilo lililotokea mwanzoni mwa mwaka huu, vipande vya vioo vilimjeruhi jirani yake na kupelekea apoteze damu nyingi.

Mahakama ya Hagerstown, Maryland nchini Marekani ikitoa hukumu ya kesi hiyo wiki hii, imemuona Melissa kuwa ana hatia ya kuvunja, kuiba na kufanya shambulio la kudhuru mwili.

Mahakama ilitupilia mbali utetezi wa Melissa kuwa aliamini kwamba analazimika kuingia ndani ya nyumba ya jirani yake ili kumuokoa mama yake na hakujua kama alikuwa akihatarisha maisha ya jirani yake.

Melissa huenda akahukumiwa kwenda jela miaka 23

No comments:

Post a Comment