KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 10, 2010

Seif aapishwa


JANA Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilimpata makamu wa kwanza wa rais kwenye serikali ya mseto na kuapishwa rasmi.

Maalim Seif Sharif Hamad atakuwa makamu wa kwanza na Makamu wa Pili kuteuliwa na Rais Shein ni Balozi Seif Ali Iddi wote kwa pamoja walikula kiapo jana cha utii na uaminifu cha kulitumikia taifa la Zanzibar vyema katika serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar.

Viongozi hao wapya waliapishwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein katika Ikulu ya visiwani humo.

"Mimi Seif Sharif Hamad naapa nitakuwa muaminifu kwa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano, nitaitumikia Zanzibar kwa moyo wangu wote katika majukumuyangu ," Eewe MWenyezi Mungu nisaidie” aliapa Seif

Naye Balozi Idd aliapa hivyohivyo akia tayari kuongoza wananchi wa visiwani humo

No comments:

Post a Comment