KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, November 11, 2010
Siku ya choo bora kuanza leo
MAADHIMISHO ya Wiki ya Choo Bora kuanza leo na Tanzania maadhimisho haypo yatafanyika mkoani Tanga.
Tamati ya maadhimisho hayo ni Novemba 19, mwaka huu ambapo maadhimisho hayo yanalenga matmizi ya usafi wa vyoo na kue;lmsiha jamii juu ya kulinda vyoo hivyo ili kuondoa magonjwa yanayopatikanda na humo.
KAtika maadhimisho hayo yaataasa na kuelimsiha jamii juu ya ujengaji holela wa vyoo usiozingatia kanuni za afya na miundombinu kwa ujumla.
Ofisa Afya Mkuu Mazingira, Bi. Mary Swai,alisema kuwa maeneo ya mijini ndio kunakotokea athari kubwa juu ya vyoo hivyo na kuwa na matatizo sugu yanayohitaji ufumbuzi wa haraka.
Alisema Jiji la Dar es Salaam ni moja ya mikoa iliyoathirika kwa uchafu uliokithiri kwa kiasi kikubwa kutokana na ongezeko la watu, huku kukiwa hakuna miundombinu inayokwenda sambamba na ongezeko hilo na kutojali matumizi sahihi ya vyoo hivyo kuongeza idadi ya magonjwa ya milipuko.
Alisema kinyesi cha binadamu kikitupwa isivyo sahihi kinaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya kama vile kipindundu, magonjwa ya kuhara, homa ya matumbo na minyoo na mengine mengi.
Hivyo maadhimisho ni pamoja na kukumbusha wananchi na halmashauri mbalimbali nchini kujenga vyoo sahihi hasa maeneo yanayoonekanea kuna mkusanyiko wa watu wengi kama vile stendi za mabasi, sehemu za starehe na kuaguliwa nat imu maalum ya halmashauri husika juu ya matumizi sahihi ya vyoo hivyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment