KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Mahujaji Watapeliwa, Wakwama Uwanja wa Ndege


MAHUJAJI wapatao 20 wamejikuta wamekwama uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere wa Dar es Salaam baada ya safari yao kuingia doa kwa kufanyiwa uhuni na taasisi ya Taibah na kutapeliwa fedha zao.
Mahujaji hao walilipa fedha zao katika taasisi hiyo ya kidini kwaajili kufanya safari yao ya kwenda Hijja Makka na badala yake walijikuta wakikwama kwenda safari hiyo kwa kukosa ushirikianao toka kwa taasisi hiyo.

Mahujaji hao walikuwa wasafiri kwa ndege za mashirika ya ndege ya Egypt na Ethiopia.

Kila hujaji mmoja alilipa kiasi cha fedha kilichopangwa na taasisi hiyo lakini walishindwa kusafiri jana baada ya kufika uwanja wa ndege na maafisa wa mashirika hayo ya ndege kudai hawana taarifa kutoka kwa taasisi hiyo.

Wakiongea kwa masikitiko mahujaji hao huku kila mmoja akiwaza kiasi kikubwa cha pesa alichokitoa kwa ajili ya safari hiyo, walidai hawaamini macho wala masikio yao kwa kitendo walichofanyiwa cha ukatili cha kukwamishwa safari yao hiyo muhimu.

"Tulihangaika kuitafuta na kuisaka nauli ya kwenda kujihi na leo pesa zetu hazijulikani zilipo", alisema mmoja wa mahujaji hao watarajiwa.

"Mimi nimelipa kwenye taasisi hii dola zipatazo elfu tatu na mia moja", alisema hujaji mmoja huku mwingine akidai kutoa kiasi cha pesa shilingi milioni hamsini kwaajili ya kugharamia safari hiyo na chakula wakiwa katika hija hiyo.

Hata hivyo juhudi za Nifahamishe.com ziligonga mwamba katika kuhakiki malalamiko ya mahujaji hao ni sahihi ama la baada ya ofisi za taasisi hiyo kufungwa na hakuna mtu yoyote aliyekuwa katika ofisi hizo huku ikidaiwa wamekimbia.

Wakati huo huo mahujaji hao walidai kuwa baadhi ya mahujaji wenzao walikamatwa na polisi baada ya kuonekana kuwa na hati feki za kusafiria zilizotolewa na taasisi hiyo

No comments:

Post a Comment