KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, November 19, 2010
Polisi wahofia mlipuko New Zealand
Picha za awali za mlipuko uliotokea zimechapishwa lakini polisi wanahofia usalama wa eneo hilo
Wafanyakazi wa mashirika ya uokoaji nchini New Zealand wamechapisha picha zilizonaswa na mtambo wa roboti zinazoonyesha mlipuko mkubwa uliotokea ndani ya mgodi wa Pike River.
Kiongozi wa shughuli za uokozi superintendent Gary Knowles, amesema sio salama kuwatuma waokoaji ndani ya mgodi huo ikiwa haijabainika kuwa gesi inayotoka ndani ina sumu au la.
Majaribio ya kutathmini hali katika mgodi huo yanaendelea baada ya mtambo wa pili wa roboti kutumwa ndani ya mgodi huo baada ya ule wa kwanza kuharibika.
Polisi wamesema wana matumaini ya kuwapata wachimba migodi 29 waliokwama ndani tangu ijumaa wakiwa hai ingawa wamejiandaa kuwapata wengine wakiwa wamefariki dunia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment