KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, November 19, 2010
Bemba kujibu tuhuma za uhalifu wa kivita
Waasi wa kundi lake la MLC walitekeleza Uhalifu nchini CAR
Kesi ya aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jean Pierre Bemba inatarajiwa kuanza baadaye leo, mjini the Hague, Uholanzi.
Bemba anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu.
Kesi yake inahusiana na visa ambavyo vilitekelezwa na waasi wa kundi lake la MLC dhidi ya raia katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2002 and 2003.
Bemba alikuwa makamu wa rais wa Congo, na ni mmoja wa kiongozi wa ngazi za juu barani Afrika
kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC.
Upande wa mashtaka unadai kuwa alishindwa kudhibiti vikosi vyake wakati vilipotekeleza ubakaji kama silaha moja ya vita. Bwana Bemba amekanusha mashtaka hayo yanayomkabili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment