KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Mgao maji waja rasmi



MAMLAKA ya Maji safi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco), imesema inatarajia kuanza kutoa mgawo wa maji unatarajiwa kuanza rasmi Novemba 25, mwaka huu.
Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Bi. Mary Lyimo alsiema, hatua hiyo inakuja kutokana upungufu wa maji kwenye vyanzo vikuu kwa Jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo.

Alisema kina cha maji kutoka Ruvu juu kiko chini sna na hiyo ndio sabau itayosababisha kuanza mgao huo kwa kuwa mamlaka hiyo haitakuwa na uwezo wa kusambaza maji kama kawaida kwa kuwa kina hicho kimeonekana kukauka.

Alisema vyanzo vya uzalishaji maji vya Jiji la Dar es Salaam kutoka Mto Ruvu, umepungua kutoka asilimia 84 hadi kufikia 59

Lyimo alisema watakaoathirika siku ya Jumatatu ni wale wa maeneo ya Ubungo, Urafiki, Sinza Mabibo, Shungashunga na Manzese.

Jumanne wataathirika wakazi wa maeneo ya Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Mwananyamala, Upanga na Ikulu.

Jumatano wataatirika wakazi wa maeneo ya Buguruni, Mburahati, Kigogo Luhanga, Bonde la Msimbazi na

Alhamisi ni Ali Maua, Chang’mbe, Keko, City Center na Kariakoo

Ijumaa ni Goba, Mbezi juu, Makonde, Salasala, Bunju A, Bunju B, Mbweni, Dovya, Boko, Kwa Masista na Mabwawa ya chumvi

Hata hivyo mbali na kuanza mgao huo maeneo mengi ya jiji la Dar yameonekana kukosa maji.

Hivyo aliwataka wakazi hao wawe wavumilivu kwa usumbufu huo kwa kuwa maji hayatoshi kusambaa kwa maeneo yote kw siku moja

No comments:

Post a Comment