KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 1, 2010

Mwananyamala wagoma kuondoka vituoni, waondolewa kwa mabomuKATIKA hali ya wananchi kuwa na kiu na matokeo yao ya uchaguzi katika kata zao, wakazi wa mwananyamala Kisiwani, Mchangani, kwa Kopa jana walilazimika kuondolewa kwa mabomu ya machozi baada ya wakazi hao kugoma kuondoka vituoni kusubiri matokeo.
Askari wa Kutuliza Ghasia [FFU] walitinga maeneo hayo baada ya wakazi hao kugoma kuondoka vituoni kwa madai wanasubiri matokeo hali ambayo jeshi hilo kulazimika kutuma kikosi chake kuwatawanya watu hao .

Katika zoezi la kuwatawanya watu hao baadhi ya watu wannne ambao walishuhudiwa na nifahamishe muda mchache baada ya zoezi hilo kumalizika walijeruhiwa katika zoezi hilo la kutuliza ghasia.

Kabla ya zoezi hilo wakazi hao waliamuriwa waondoke vituoni hapo lakini walionekana kuwa wakaidi kwa madai wanalinda kura zao zisiibiwe na kuonekana wanachochea fujo na kuonekana mamluku wa vyama.

Kabla ya zoezi hilo gari la polisi liwatangazia wananchi hao kusogea mita 200 kutoka vituoni lakini walionekana kukaidi na magari ya jeshi hilo yaliingia katika vituo hivyo mfululizo na kwua na silaha na mabomu ya machozi huku moja likiwa na maji ya upupu.

Hata hivyo maeneo hayo yalionekana kuwa na fujo hadi nifahfamishe inaondoka viutoni hapo majira ya saa 12 jioni wananchi walijiandaa kwa kulala vituoni hapo hadi matokeo kutangazwa.

Vituo vingine vilivyoponekana kuwa na washabiki ni maeneo ya Temeke wananchi walikaa mita kadhaa kusubiria matokeo hayo ambayo wamedai wamesitisha shughuli zao kwa ajili ya matokeo hayo

No comments:

Post a Comment