KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 1, 2010

Matukio Yaliyojiri Wakati wa Uchaguzi Tanzania


Wapiga kura wakihakikisha majina yao kwenye kituo cha kupigia kura


Uchaguzi umeisha na kura zimeanza kuhesabiwa, uchaguzi umemalizika salama ingawa kulikuwa na matukio ya hapa na pale yaliyotia dosari zoezi la upigaji kura.
Mamilioni ya Watanzania walijitokeza jana kuzitumia kura zao kuwachagua viongozi watakaoliongoza taifa kwa miaka mitano ijayo.

Zoezi zima la uchaguzi lilimalizika salama ingawa kulikuwa na matukio madogo madogo yaliyotia dosari zoezi hilo.

Huko Kondoa Kaskazini, kituo cha kupigia kura cha Belabela kilichomwa moto na wafanyabiashara ambao hawakufurahishwa na hatua ya kituo cha kupigia kura kuwekwa kwenye eneo lao la biashara.

Visiwani Zanzibar, vituo kadhaa vya kupigia kura havikuwa na karatasi za
kupigia kura za rais na wabunge wa muungano.

Huko Arusha, daftari la wapiga kura lenye karatasi 400 katika kituo cha kupigia kura katika Shule ya msingi Sombetini lilipotea katika mazingira ya kutatanisha na kupelekea msimamizi wa kituo cha kupiga kura atiwe mbaroni na polisi.

Huko Lindi, wafuasi wa CUF waliokusanyika kwenye vituo vya kupigia kura kusubiri matokeo baada ya zoezi la kupiga kura kuisha, walitimuliwa na polisi wenye silaha

No comments:

Post a Comment