KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 10, 2010

Msoga wampongeza JK


WAKAZI na wanavijiji ya Kata ya Msoga wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani jana waliandaa sherehe za kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuchaguliwa tena kwa mara nyingine kuongoza nchi ya Tanzania.
Wanakijiji hao jana walimpongeza mwanakijiji mwenzao huyo na kumkaribisha nyumbani kutokana na furaha yao ya ndugu yao huyo kupata ushindi huo.

Sherehe hizo zilizofanyika kijijini humo ni kumuenzi kiongozi huyo kwa kuwa kijiji hicho ndicho alichozaliwa Rais huyo na kulelewa katika kijiji hicho.
Sherehe hizo ziliambatana na ngoma za asili ya mahali hapo na Raisi huyo kujumuika kusakata ngoma hizo na kuungana na wanakijiji wenzake hao jambo liliwavutia watu wengi kuonbekana kucheza ngoma hizo.

Wanakijiji hao walimpongeza ndugu yao huyo ka kuwa aliweza kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi wa mwaka 2005 -2010 na ndio sababu ya kupata ushindi huo.

Rais kikwete aliwashukuru wanakijiji hao kwa kumuunga mkono tokea safari zake za siasa kuanza kutafuta Ubunge wa Jimbo la Chalinze na hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mbali na kumpongeza Kikwete pia waliweza kumpa shukrani za dhati mama Salama Kikwete kwa juhidi zake za kuwa nsambamba na mumewe huyo toka mchakato huo wa uombaji kura hadi kumalizika kwa uchaguzi

No comments:

Post a Comment