KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, November 10, 2010

Papo hapo kwa kukanyagwa na lori la bia


KIJANA mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja wala umri wake, asubuhi ya leo amejikuta ndio mwisho wake wa kuishi duniani baada ya kukanyagwa na matairi ya lori linalosambaza bia huko maeneop ya Karume Ilala jijini Dar es salaam.
Kijana huyo ambaye ni dereva wa pikipiki, alipokuwa maeneo hayo ya karume akiwa na usafiri wake huo alijaribu kumkwepa mtembea kwa miguuu apite, pikipiki hiyo ilitereza tairi lake na kulala na wakati akijiatahidi kuokoa maisha yake huku gari jingine lilikuwa likija nyuma nyake.

Hata hivyo kijana huyo hakufanikiwa na wakati akitaka kukwepa gari hilo alijikuta akiingia uvunguni mwa lori na kukanyagwa na matairi maeneo mbavu, kichwani huku bila dereva wa lori kujua ka kuwa lilikuwa likienda taratibu.

Hivyo kijana huyo aliweza kupoteza maisha yake papohapo, kwa kuwa matairi ya trela la nyuma yote kuishia kichwani mwake.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 3 :48 leo asubuhi eneo la Karume na kuacha majonzi na masikitiko maeneo hayo kutokana kijana huyo japo na kuiwa na elementi kichwani lakini haikusaidia na kupoteza uhai na kuahchaq pikipiki nay eye kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti amana.


Lori lililomkanyaga lilikuwa ni la kampuni ya bia Tanzania Breweries na lori hilo lilikuwa karibu na kuingia kiwandani hapo kwa ajili ya shughuli za kila siku za kampuni hiyo

No comments:

Post a Comment