KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Mashoga Walana Denda Mbele ya Papa


Mamia ya mashoga wa nchini Hispania walinyonyana ndimi kwa dakika tano mbele ya Papa Benedict XVI katika kupinga kauli zake za kupinga ndoa za wanaume kwa wanaume.
Ziara ya Papa Benedict XVI nchini Hispania imekumbana na vioja vya mashoga wa nchini humo ambao waliamua kunyonyana ndimi mbele yake ili kupinga kauli zake za kupinga utoaji mimba na ndoa za watu wa jinsia moja.

Wakati gari la Papa ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 83 lilipokuwa likipita barabarani mbele ya maelfu ya waumini wa kanisa katoliki mjini Barcelona, mamia ya mashoga na wasagaji walinyonyana ndimi hadharani kwa takribani dakika tano ili kuonyesha upinzani wao kwa kanisa katoliki.

Hata hivyo pamoja na mashoga kuonyesha upinzani wao, Papa katika hotuba yake aliendelea kukemea ndoa za jinsia moja na utoaji mimba.

Papa alisema kuwa sheria za Hispania zimewapa nafasi wanawake kutoa mimba kirahisi na pia wanaume kuwaoa wanaume wenzao.

Papa aliendelea kusema kuwa kanisa katoliki litaendelea kukemea hali zozote zinazopingana na maisha asilia ya binadamu katika kujenga familia bora

No comments:

Post a Comment