KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Baada ya Kuambukizwa Ukimwi, Polisi wa Kenya Awaua Watu 10


Afisa mmoja wa polisi nchini Kenya amewaua watu 10 kwa kuwapiga risasi wakati akimtafuta mwanamke aliyemuambukiza ukimwi.
Afisa wa polisi wa nchini Kenya aliyedai anamwinda mwanamke aliyemuambukiza ukimwi, alivamia baa tatu katika kitongoji cha Siakago kilichopo maili 90 kaskazini mwa Nairobi na kuwaua watu 10 wakiwemo maafisa wenzake wawili wa polisi.

Afisa huyo ambaye ana umri wa miaka 30 na ushee, alifanya mauaji hayo jioni ya siku ya jumamosi wakati akimtafuta mpenzi wake ambaye alidai amemuambukiza HIV, alisema kamishna wa polisi wa wilaya, John Chelimo.

"Inasemakana kuwa afisa huyo alikuwa akimtuhumu msichana mmoja kuwa amemuambukiza HIV, alitoka jioni kwenda kumtafuta kwenye baa lakini hakumpata", alisema mkuu wa polisi wa eneo hilo.

Afisa huyo wa polisi alifanya mashambulizi yake kwenye baa tatu tofauti.

"Wakati milio ya risasi iliposikika, polisi wawili walimfuata afisa huyo wa polisi na kumuita kwa jina lake, hakuitikia na badala yake aliwapiga risasi na kuwaua hapo hapo", alisema Chelimo.

Afisa huyo wa polisi aliwaua jumla ya watu 10 ambapo wanawake walikuwa wawili na wanaume walikuwa wanane.

Baada ya mauaji hayo, mamia ya watu wenye hasira waliandamana mbele ya kituo cha polisi cha Siakago kwakuwa mauaji hayo yalifanyika mbele ya kituo cha polisi.

"Mauaji yalifanyika karibu sana na kituo cha polisi", alisema mwanaume mmoja ambaye binti yake ni mmoja wa watu waliouliwa na afisa huyo wa polisi.

"Hapa Siakago hakuna usalama kabisa ", alisema mwanaume huyo na kuongeza "Mtu anaweza akawapiga risasi watu 20 hadi 30 bila ya polisi kuchukua hatua yoyote".

Taarifa ya polisi ilisema kuwa afisa huyo ametupwa rumande akisubiri kufikishwa mahakamani

No comments:

Post a Comment