KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Viongozi wa G20 wakutana Korea Kusini


Suala la thamani ya sarafu za nchi hizi tajiri duniani huenda likatawala mijadala kwenye mkutano huu.

Marekani na China, wote wanalaumiwa kuwa wanamazoea ya kupunguza thamani ya sarafu zao ili kufanya zile zingine kuto mudu ushindani katika soko la ubadilishanji wa pesa.

Hata hivyo nchi hizi zinatetea hatua zao za kuthibiti thamani ya sarafu zao na hili huenda likawa suala gumu kutatua.

Marekani inatetea msimamo wake kwa kuwa kiwango cha riba nchini humo kiko chini na pia mfumo wa sera za benki kuu nchini humo, US federal Reserve unawachochea wawekezaji kuuza sarafu hiyo iliwapate faida kubwa katika sehemu zingine.

Thamani kushuka

Mfumo huu wa benki kuu ya Marekani, unafuatwa kutokana na kuwa uchumi wa nchi hiyo unakuwa kwa kasi ndogo na huenda sera hiyo isibadilike hadi pale uchumi huo utakapo kuwa imara.

China nayo inasema, uchumi wake unaingiliana na ule wa Marekani na kwa maana hiyo, thamani ya sarafu yake inalazimika kushuka sana ikilinganishwa na zingne duniani.

Lakini Marekani ndio inayoongoza kulalamikia hatua hiyo, ikisema kutokana na hatua hiyo China inakuwa na nafasi bora zaidi ya ushindani kwenye soko ikilinganishwa na nchi zingine.

Hata hivyo, China haina haraka kubadili mfumo wake, kwa sasa imesema itaruhusu soko la ubadilishanaji wa sarafu liamue kuhusu thamani ya pesa zake lakini pia itawalinda wawekezaji nchini humo wanaouza bidhaa zao nje ya nchi kutokana na athari za kuongezeka kwa thamani hiyo.

Afrika inawakilishwa na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Bingu wa Mutharika wa Malawi na mwenyekiti wa Nepad na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi

No comments:

Post a Comment