KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Jitokezeni kwa wingi kupiga kura - Kiir


Salva Kiir akijiandikisha kupiga kura




Kiongozi wa Sudan Kusini Salva Kiir amewataka wananchi wake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kupiga kura ya maoni ya kujitawala yenyewe au la itakayofanyika mwezi Januari.




Bw Kiir alikuwa akizungumza mbele ya umati wa mamia ya watu katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, baada ya uandikishaji kuanza.

Kura ya maoni ni sehemu ya makubaliano ya amani ya mwaka 2005 ya kumalizamiaka mingi ya mapigano ya Sudan Kusini na Kaskazini.

Pande hizo mbili zilikubaliana kuainisha mpaka kati ya Kusini na Kaskazini, na pia kuruhusu wafugaji kulisha upande wa Kusini





Salva Kiir


Makubaliano hayo pia yanajumuisha kuruhusu raia wote wa Sudan kuwa na haki ya kuishi Kusini au Kaskazini.

Bw Kiir, ambaye ni kiongozi wa zamani wa kundi la waasi, na ambaye anaongoza serikali ya sasa ya Sudan Kusini, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kujiandikisha.

"Kura ya maoni hutokea mara moja tu. Watu lazima wajitokeze kwa wingi, vinginevyo itamaanisha watu walipigana na kufa bila sababu," amesema Bw Kiir.

wanaharakati wakiwa na vipaza sauti wamepita katika mitaa ya Juba, wakiwataka wakazi kujiandikisha kupiga kura.

Wachambuzi wa mambo wanatarajia kuwa wananchi wa Kusini watapiga kura upande huo kujitenga na kusababisha taifa hilo kubwa la Afrika kuganwanyika mara mbili

No comments:

Post a Comment