KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

CCM yaanza tathmini uchaguzi mkuu uliopita


Venance George, Morogoro
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilombero, kimeanza thatmini na kujipanga upya kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa chama hicho na jumuiya zake utakaofanyika mwaka 2012.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kilombero, Robert Kerenge, alisema hatua hiyo inakwenda sambamba na kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita.

Kerenge alisema tathmini hiyo inaanzia ngazi ya tawi, kata hatimaye wilaya na vikao vya tawi na kata vitafanyika kati ya Novemba 16 hadi 22, mwaka huu.
Alisema vikao vya wilaya vitafanyika kati ya Novemba 24 hadi 29, mwaka huu na lengo ni kupitia taarifa za matawi na kata hatimaye kupeleka taarifa mkoani.

Katibu huyo aliomba wanachama na viongozi ngazi zote kujipanga kwa ajili ya kuimarisha chama kwani, huu ni muda wa kufanya kazi za chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuhusu makundi ndani ya chama hicho katika wilaya hiyo, Kerenge alikanusha kuwepo kwa makundi na kwamba yalikuwepo madogo ambayo hayakuwa na tija zaidi, hivi sasa yamevunjwa na nguvu zote kuelekezwa katika maandalizi ya uchaguzi.
Alisema anaamini kama umoja ukiwepo kwa wanachama wote ndani ya chama hicho, ana imani ushindi wa kishindo utakuwepo chaguzi zote zinazokuja.

Katika uchaguzi uliopita kwa ngazi zote CCM Wilaya ya Kilombero, ilifanikiwa kupata kura nyingi kwa upande wa urais na mbunge wake akifanikiwa kushinda ingawa walipoteza kata nne kati ya 23

No comments:

Post a Comment