KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Kikwete awatema hawa!



KATIKA baraza lake jipya la mawaziri alilolotangaza jana, Rais Kikwete amewacha baadhi wa mawaziri aliokuwa nao katika awamu yake ya kwanza ya uongozi na kubadili baraza hilo katika sura mpya.

Kikwete amemuacha aliyekuwa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msola, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu a Rais Muungano, Mohamed Seif Khatib.

Wengine aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, aliyekuwa Waziri wa Aradhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati.

Waliokuwa manaibu waziri katika wizara mbalimbali waliotemwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Maua Daftari, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Miundombinu, Ezekiah Chibulunje.

Wengine waliopoteza nafasi zao baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu kukosa ubunge ni aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Sera, Uratibu na Bunge, Philip Marmo , aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Aisha Kigoda, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza .


Wengine waliopoteza nafai zao ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya NDani ya Nchi, Lawrence Masha, aliyekwua Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera , aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta.


Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk. James Wanyancha, na aliyekuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala.

Hao ndio waliopoteza nafasi zao katika baraza hili jipya la mawaziri lililotangazwa jana, majaira ya saa 6 mchana, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Na Rais jana alionekana kuwaacha wanahabari hoi mara baaada ya kumaliza kutaja majina wa mawaziri hao alitoa shukrani na kuinuka na kukataa kuulizwa maswali na kuacha wanahabari wakiwa katika butwaa

No comments:

Post a Comment