KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, November 19, 2010
Chadema si shwari
CHAMA cha Maendeleo na Demokrasia [CHADEMA] kimeonekana kuwakatika wakati mgumu kutokana na viongozi wa juu, wabunge kutofautiana na kuwa na mgawanyiko kutokana na kitendo chao cha kususia hotuba ya Rais Kikwete bungeni.
Hali hiyo imetokea ni muda mchache tu mara baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya urais na katibu mkuu wa chama hicho, Wilbrod Slaa kutngaza kua hawatambui matokeo hayo.
Hali hiyo ndiyo iliyofanya baadhi ya wabunge wa chama hicho kususia pia hotuba ya Rais Kikwete, alipokuwa akizindua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 18, Dodoma na kuahca gumzo kubwa ndani ya bunge hilo na kuonekana kudharau bunge pamoja na
Rais wa nchi kutokana na kitendo hicho.
Hivyo kutokana na katibu huyo kutoa kauli hiyo wabunge wa chama hicho walilazimika kususia shughuli za kiserikali ikiwemo na kutohudhuria kuapishwa kwa Waziri Mkuu Pinda Kimwaga na kutamka kuwa hawako tayari kuwa katika baraza la mawaziri hata kama Rais atafanya uteuzi ndani ya chamda hicho.
Hatua hiyo ilisababisha mgawanyiko wa wazi, kwa baadhi ya wabunge kutoshiriki ususaji huo na kutoa sababu zao walizoona ni za msingi akiwemo na mbunge wa Kigoma Kaskazini. Kabwe Zitto kutoshiriki katika mgomo huo jambao linalozua mizozo ndani ya chama hicho.
Kufuatia hali hiyo nae Mwenyekiti wa Chama hicho wa Mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala akatangaza kujiuzulu ghafla wadhifa huo ili kupisha uchunguzi wa kina juu ya tuhuma zilizoelekezwa kwake.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Bi. Leticia Musori, alitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na NCCR-Mageuzi. .
Baadhi ya wabunge wa chama hicho na walioweza kuongea na maishani walijitetea kwa kudai kwamba, wao walifata mkumbo kwa kuogopa kutengwa na chama hicho lakini baadhi hawakufurahishwa na kitendo cha kutoka nje ya ukuimbi wa bunge
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment