KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 3, 2010

Jimbo la Ukonga, Segerea utata



JIMBO la Ukonga na Segerea linaonekana kuwa na utata katika kutoa matokeo kwa sababu tofauti kati ya sababu hizo ni kupotea kwa kura zilizopigwa katika masanduku.,


Hali hiyo imewafanya wakazi wa maeneo ya ,majimbo hayo kupatwa na wasiwasi kwa kutolewa kwa matokeo ambayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Ilala, Bw. Fuime Gabrieli alisema kuwa, zoezi la kuhesabu kura hizo bado halijakamilika kutokana na baadhi ya masanduku yaliyoletwa kwa kuhesabiwa kukutwa bila kura zilizopigwa.

Sababu nyingine alisema ni kucheleshwa kwa masanduku ya kura kutoka katika vituo tofauti vya majimbo hayo.

Alisema tatizo iliyosababisha hayo ni wasimamizi wa vituo wakati wanakusanya masanduku hayo kuletwa ka kuhesabiwa inaonekana walisahau mahali walipoweka kura hizo wakati wanasafirisha na bado wasimamizi wanatafuta walipohifadhi kura hizo .

Majimbo hayo ni kati ya majimbo yanayosisimua na awlai kulikuwa na jimbo moja la Ukonga na sasa limegawanywa na kuwa majimbo mawili ya Ukonga na Segerea.

No comments:

Post a Comment