KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 3, 2010

Dk Ali Mohammed Shein wa Chama cha Mapinduzi CCM amekuwa rais mpya wa Zanzibar kwa miaka mitano ijayo


Dk Ali Mohammed Shein wa Chama cha Mapinduzi CCM amekuwa rais mpya wa Zanzibar kwa miaka mitano ijayo



Dk Ali Mohammed Shein wa Chama cha Mapinduzi CCM amekuwa rais mpya wa Zanzibar kwa miaka mitano ijayo baada ya kumbwaga mpinzani wake mkubwa Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF kwa ushindi wa asilimia 50.1.
Chama cha Mapinduzi CCM kitaendelea kuitawala Zanzibar kwa miaka mitano ijayo baada ya mgombea wake wa urais visiwani Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein kushinda uchaguzi kwa kupata asilimia 50.1 ya kura zote.

Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF ambaye hii ni mara yake ya nne kugombea urais wa Zanzibar na kushindwa, alijipatia asilimia 49.1 ya kura zote.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar, ZEC, Salum Kassim Ali alisema kuwa jumla ya watu 364,924 walipiga kura katika majimbo 50 ya visiwani humo.

Maalim Seif alipata jumla ya kura 176,338 wakati Dk Shein alijizolea jumla ya kura 179,809.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Maalim Seif alitangaza kuyakubali matokeo na kusema kuwa hakuna mshindi wala aliyeshindwa katika uchaguzi huo.

"Watu pekee waliopata ushindi ni Wazanzibar", aliongeza Maalim Seif.

Dk Shein kwa upande wake, aliwapongeza wapinzani wake na kuwashukuru Wazanzibar kwa kumuamini na kumpa heshima ya kuiongoza Zanzibar

No comments:

Post a Comment