KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 19, 2010

Hausigeli Alazimishwa Ameze Misumari na Bosi Wake


Katika kesi ya tatu ya kuteswa kwa wafanyakazi wa ndani katika nchi za kiarabu, mfanyakazi wa ndani nchini Jordan anapatiwa matibabu baada ya kulazimishwa kumeza misumari sita na bosi wake.
Ndani ya kipindi cha miezi mitatu, mfanyakazi mwingine wa kike wa tatu toka Sri Lanka anapatiwa matibabu baada ya kulazimishwa kumeza misumari sita na bosi wake kama adhabu kwa kutofanya vizuri kazi zake.

Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la D.M. Chandima alikimbilia kwenye ubalozi wa Sri Lanka mjini Amman kushtaki baada ya bosi wake kumlazimisha kumeza misumari.

"Tunasubiria taarifa kamili ya daktari kabla ya kuchukua hatua yoyote", alisema afisa mmoja wa ubalozi huo.

Tukio hilo limekuwa ni tukio la tatu la wafanyakazi wa ndani kuteswa katika nchi za kiarabu.

Mwanamke mwingine naye raia wa Sri Lanka aliyekuwa akifanya kazi nchini Kuwait alimshtaki bosi wake ambaye aliipigilia misumari 14 kwenye mwili wake baada ya kudai mshahara wake wa miezi sita ambao hakulipwa.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 38, alifanyiwa upasuaji nchini Sri Lanka kuiondoa misumari hiyo toka kwenye mwili wake.

Mwezi wa nane mwaka huu, mwanamke mwingine aliyekuwa akifanya kazi nchini Saudi Arabia naye alilalamika baada ya muajiri wake kuipigilia misumari 24 kwenye mikono, miguu na paji lake la uso kama adhabu kwa kutofanya vyema kazi zake.

Mwanamke huyo naye alifanyiwa operesheni nchini Sri Lanka kuondolewa misumari hiyo.

Raia Milioni 1.8 wa Sri Lanka wanafanya kazi ughaibuni ambapo asilimia 70 kati yao ni wanawake wanaofanya kazi za ndani katika nchi za mashariki ya kati

No comments:

Post a Comment