KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 10, 2010

Ili Kumlinda Obama, Nazi Zaangushwa Toka Kwenye Minazi IndiaIli kumlinda rais wa Marekani Barack Obama anayefanya ziara yake nchini India, serikali ya India imeamua kuangua nazi zote toka kwenye minazi iliyo karibu na majengo ambayo Obama atayatembelea.
Katika kujiandaa kumpokea kwa mara ya kwanza rais wa Marekani, Barack Obama, serikali ya India imeangua nazi zote toka kwenye minazi iliyopo karibu na majengo ambayo Obama atayatembelea mjini Mumbai.

Obama anawasili leo jumamosi nchini India katika hatua yake ya kwanza ya ziara zake katika bara la Asia.

Pamoja na ulinzi mkali kuwekwa kama ilivyotegemewa, maafisa wa serikali ya India wameamua pia kuchukua hatua zaidi kwa kumlinda rais huyo wa Marekani hata kwa hatari zitokenazo na mimea.

Nazi zote toka kwenye minazi yote inayolizunguka jengo la ukumbusho la Gandhi zimeangushwa chini ili kumlinda Obama.

Jengo hilo ni mojawapo ya sehemu tano ambazo Obama atazitembelea mjini Mumbai. Katika sehemu zote hizo hatua sawa za ulinzi zimechukuliwa.

"Kwanini tubahatishe?, tumewaagiza maafisa husika kuziangua nazi zote toka kwenye minazi iliyo karibu na jengo hili", alisema mkurugenzi wa jengo la Mani Bhavan ambalo Mahatma Gandhi aliishi wakati wa kupigania uhuru wa India toka kwa Uingereza.

Wiki iliyopita maafisa wa Marekani walilifanyia uchunguzi jengo la Mani Bhavan pamoja na sehemu zingine ambazo Obama atazitembelea.

Obama atazitembelea pia nchi za Indonesia, South Korea, Japan na China katika ziara yake ya siku 10 barani Asia

No comments:

Post a Comment